MAANDALIZI YA MUHULA MPYA 2015
Malengo yetu bado
yanasimama palepale kuwa ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwa mitihani ya
ndani pamoja na mitihani ya mwisho ya taifa kwa kidato cha nne,hivyo
sisi kama Kikanda sekondari tumejiandaa vya kutosha ili kutoa elimu
iliyo bora na inayokidhi mahitaji ya jamii yetu ya Kitanzania kutokana
na mwongozo wa mtaala wetu.Kama isemavyo ratiba tunategemea kufungua
shule tarehe 13/07/2015 hivyo tunaomba wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi wa
Kikanda Sekondari kuhimiza vijana wao kuwahi shule ili wasipitwe na
masomo ambayo yamepangwa kwa mujibu wa ratiba.
WAZAZI
WAZAZI
ZINGATIA-mzazi unapaswa kumueleza kijana wako umuhimu wa elimu na kuwa na
nidhamu bora katika kipindi chote atakachokuwa shuleni
RATIBA YA MUHULA
Tunategemea kuweka ratiba ya muhula mzima kutoka kufinguliwa shula mwezi
ujao mpaka kufungwa hapo baadae mwezi wa 12 /2015 ili kusaidia wewe mzazi na
mwanafunzi kuweza kufahamu ratiba nzima ya masomo
Ahsanteni
MENGINEYO
Endelea kutufuatilia hapa Kikandasecondary.blogspot.com,facebook.com.au
twitter.com ili uweze kupata ratiba zetu,matokeo ya mitihani yetu ya
ndani kama weekly test na mid term test.Michezo mbalimbali na shughuli
nyinginezo za shule katika muhula huu mpya.
Natanguliza shukurani
Mkuu wa Shule>Kikanda sekondari-Kilwa
No comments :
Post a Comment