Katika hali ya kuongeza hamasa ya usomaji na kufanya vizuri
kwa wanafunzi katika masomo yao,Kikanda sekondari imeanza kutoa zawadi kwa
wanafunzi wanaofanya vizuri katika mihula ya mwaka hii ni pamoja na kutoa
zawadi kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana waliofanya vizuri,lengo ni
kuboresha elimu na kuongeza hamasa kwa wanafunzi.
Hivyo tunawaletea tukio zima kwa ufupi juu ya utoaji tuzo
hizo ambazo mwenyekiti wake na ambaye pia ni mkuu wa shule alikabidhi zawadi
hizo kwa wanafunzi hao
2.4, Mkuu wa shule
akimkabidhi mwanafunzi Haji Magina
zawadi baada ya kufanya vizuri katika mitihani ya taifa kidato cha nne 2014
huku makamu mkuu wa shule akifuatilia kwa karibu tukio hilo